Huu ndio Mjengo wa Jamii ya Wahadzabe

Katika jamii ya Wahadzabe mwanamke ana jukumu la kujenga nyumba ya asili kwa ajili ya familia. Nyumba hii hujengwa kwa kutumia miti ya porini na kuzungushiwa nyasi na miba ambapo ngozi ya pofu ndio hutumika kama godoro la kulalia.

Waweza kijuliza inawezekanaje mtu kulala katika nyumba hii bila kuvamiwa na Wanyama wakali kama Simba na hata wadudu wanaotambaa kama nyoka, ng’e na wengineo?.

Dawa za mizizi inayozungushiwa kwenye nyumba na kuchanja kwenye mwili ni sehemu ya kinga dhidi ya Wanyama wakali. Yapo mengi ambayo Tanzania Safari Channel itaendelea kukuangazia mkoa huu wa Singida ambayo kwayo yamekuwa yakiitangaza Tanzania Kimataifa katika suala zima la utalii.

@emmanuel9397 📷 @elia__stephano 📷 📷