Utamaduni wa Wahadzabe

Wahadzabe huishi katika pori linalozunguka ziwa Eyasi kaskazini mwa Iramba katika wilaya ya Mkalama,Kijiji cha Munguli na kata ya Mwangeza.
Jamii hii ni wakoithan kilugha na huishi porini huku chakula chao kikiwa ni asali, Nyama, Matunda na mizizi ya porini.


Katika mgawanyo wa majukumu kwenye jamii ya Wahadzabe mwanaume kazi yake kubwa ni kutafuta chakula kwa kuwinda au kurina asali huku mwanamke akifanya shughuli za ujenzi na usagaji ubuyu kwa ajili ya familia.
Ngoma ya asili ya kihadzabe pamoja na mavazi ya asili yaliyotengenezwa kwa Ngozi za wanyama mbalimbali kunakshiwa na shanga huvutia watalii wengi kutembelea eneo hili kwani huvutiwa zaidi na mtindo wao wa maisha wa jamii hiyo kiujumla