Mambo ya kufahamu Kuhusu Chatu

Chatu ni mojawapo ya nyoka wakubwa. Tofauti na aina nyingine za nyoka, chatu hawatoi sumu (ni nyoka wasio na sumu) .Chatu wanaishi katika maeneo ya kitropiki ya Afrika na Asia.

Wanaweza kupatikana katika misitu ya mvua, savanna na jangwa.

Chatu hawashambulii wanadamu, isipokuwa wakiwa wamekasirishwa au wakiwa na msongo wa mawazo.

Chatu wanaua mawindo yao kwa kufinya mnyama mpaka aache kupumua.Baada ya kuua mnyama, hummeza kama alivyo na kila kitu isipokuwa manyoya ambayo humeng’enywa.

Muda wa mmeng’enyo wa chakula hutegemea ukubwa wa mawindo uliofanywa.

Mawindo makubwa zaidi yanaweza kumfanya nyoka ashibe kwa wiki au miezi kadhaa. Hivyo kwa wastani Chatu hula mara 4-5 kwa mwaka. Wanakula wanyama pori kama vile nyani, swala,ndege,mijusi wakubwa na viumbe wengine wakubwa kwa wadogo.

Chatu hushambulia mawindo yao kwa kuvizia. Wao kwa kawaida hujificha kwenye miti. Ingawa mara nyingi Chatu huwa chini au kwenye miti, chatu ni waogeleaji bora sana.

Chatu jike hutaga mayai takribani 12-36. Yeye hulinda mayai na kuyapa joto kwa kuyazungushia mwili wake.

Akishatotoa mayai mama huondoka kwenye kiota na kisha Chatu wachanga huanza kujitunza kutoka siku ya kwanza.

Picha hizi ni za Chatu aliyeonekana kwenye Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo ambapo kuna idadi kubwa ya Chatu wadogo kwa wakubwa.

Likes:
0 0
Views:
165
Article Tags:
Article Categories:
Education Tourism