Miti zaidi ya milioni 8.2 yapandwa mwezi wa mama

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), limeendesha kampeni ya kupanda miti nchi nzima na kufanikisha kupanda miti zaidi ya milioni 8.2.

Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC 1, Kamishna wa Uhifadhi wa TFS Profesa Dos Santos Silayo amesema, kampeni hiyo imelenga kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira.

Amesema kampeni hiyo maalum pia inafanyika ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais Samia Suluhu Hassan hii leo.

Aidha, Dos Santos amesema TFS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imejipanga kuhakikisha miti iliyopandwa inakuwa na kuleta manufaa yaliyokusudiwa kutokana na kupandwa kimkakati.

Likes:
0 0
Views:
291
Article Categories:
Education Tourism