Mti una zaidi ya miaka 200

Mti wa Mvanga ni kivutio cha asili ambacho kinapatikana kwenye Mlima Igeleke mkoani Iringa katika eneo la Kihesa Kilolo.

Mti huu una zaidi ya Miaka 200 na sifa yake kubwa ni mgumu na hauwezi kuliwa na wadudu wala kuharibiwa na unyenyenyevu ambapo hata ukikatwa na kufukiwa ardhini baada ya miaka 50 unaukuta upo vilevile haujaharibika.

Mti huu ni miongoni mwa miti michache sana inayopatikana ukanda wa Tropiki ambapo zamani ulitumika kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba na vyoo.

Likes:
0 0
Views:
369
Article Categories:
Education Tourism