Utajiri uliopo katika Hifadhi ya Msitu Geita

Mnamo mwaka 1953 Wakoloni waliutangaza kuwa kama Msitu wa Hifadhi. Msitu huu una takribani hekari 50, na unapatikana umbali unaokaribia kilometa 3 kutoka Geita Mjini.

Msitu huu una uoto wa asili, maporomoko ya maji polepole, aina mbalimbali za wadudu ikiwemo vipepeo na nyuki. Historia kubwa ya uchimbaji wa madini nayo imehifadhiwa ndani hapa, kuna mashimo makubwa yanayosemekana kuwa kati ya mashimo ya mwanzo kabisa yaliyotumika kwa uchimbaji wa madini ambayo kwa sasa yamejaa maji na kuwa kivutio kikubwa cha utalii.

Likes:
0 0
Views:
311
Article Categories:
Education Tourism