Boma la Wajerumani Manyoni

Haya ni baadhi masalia ya boma la Wajerumani waliokuwa wakifanya biashara ya kusafirisha watumwa Afrika Mashariki kati ya Karne ya 18 na 19.

Masalia ya boma hili yapo katika kijiji cha Kilimatinde wilayani Manyoni, ni moja ya eneo la kihistoria ambalo limekuwa likitembelewa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kujifunza mambo ya kihistoria yanayopatikana mkoani Singida.