Chemchemi ya maajabu Kondoa

Kilometa nne kutoka Kondoa Mji, katikati ya msitu mnene uliosheheni miti mikubwa ya kijani huku kwa mbali sauti za ndege na wadudu wanaofurahia mandhari hiyo zikisikika ipo Chemchemi ya asili Kondoa inayosemwa kuwa na maajabu ya kipekee na mengine yasiyoweza kusimuliwa.

“Sharti ni moja, usiitike utapoitwa ukiwa ndani ya eneo hili ama la itika jina la mwenzio ukisikia ameitwa,” ni masharti tuliyopewa tukiwa ndani ya eneo la chemchemi huku tukiambiwa endapo utaitwa mara tatu basi unaweza itika.

Ndani ya eneo la chemchemi hii yupo Mzee Musa Mwenda akilinda chemchemi na kufanya usafi katika eneo hilo. Anaeleza kuwa yeye si mlinzi pekee wa eneo hilo kwani wapo Chatu watatu wakubwa ambao ni nadra sana kuonekana lakini mara kadhaa ifikapo saa nne usiku huja katika eneo hilo na kukaa hadi saa 11 asubuhi.

Eneo hili Mzee Mwema analitaja kuwa na mizimu ambayo pale inapokorofishwa huja saa saba usiku au mchana na kupiga piga mabati yaliyoezekwa kwenye chemchemi hiyo lakini pia pale ambapo taratibu zitafanywa na kuwaomba msamaha basi mizimu hiyo hurudi mida hiyo hiyo usiku na kupiga vigelegele.

Kuanzia majira ya saa moja jioni ama saa mbili hadi saa mbili asubuhi chemchemi huanza kutoa maji ya uvuguvugu na kisha asubuhi hiyo hadi jioni hutoa maji ya baridi.

Kanimvutano iliyopo kwenye chemchemi hiyo ilipelekea paa la chemchemi kuezuliwa na kupaacha wazi.

Likes:
0 0
Views:
54
Article Tags:
Article Categories:
HistoryTourism