Magofu ya Engaruka yaliyobeba historia ya ustaarabu wa Mwafrika katika Kilimo

Magofu ya Engaruka ni moja ya maeneo yenye historia kubwa sana Tanzania? Miaka 500 hivi iliyopita, jamii ya wakulima ilitumia mfumo wa hali ya juu wa kilimo cha umwagiliaji.

Historia inaeleza kuwa jamii hii ilikuwa na ubunifu mkubwa licha ya udhaifu wa zana za chuma zilizokuwepo enzi hizo.

Hali ya hewa kwenye Bonde la Engaruka ni ukame kutokana na milima mirefu inayolizunguka ambayo huzuia upepo wa mvua na hivyo kusababisha mvua chache sana. Lakini bahati ni kwamba milima hiyo inatiririsha maji mengi yanayolineemesha bonde hilo.

Hali hiyo huchochea wakulima hawa kutumia njia mbadala ya kutumia maji ya mtoni ili kumwagilia mashamba yao.

Walitumia mawe kutengeneza mifereji iliyoruhusu maji kuingia kwenye mashamba yao na hatua zilichukuliwa ili kuzuia mmomonyoko wa udongo huku samadi ya ng’ombe ikitumiwa kuongeza udongo.

Kwa sababu zisizojulikana, wakulima hao waliondoka Engaruka kufikia miaka ya 1700. Sasa, karne tatu baadaye, magofu ya Engaruka yamebaki kuwa kielelezo kikubwa cha ustaarabu wa mwafrika katika kilimo.

Zipo nadharia nyingi zinazolenga kujibu Maswali mengi kuhusu Engaruka

  • Watu walioishi Engaruka walikuwa nani?
  • Walikujaje kukuza mfumo wa kilimo cha kuingia?
  • Kwanini hatimaye waliondoka Engaruka?

Tanzania Safari Channel itakuletea mwendelezo wa makala hii ya kusisimua.

Likes:
0 0
Views:
2507
Article Tags:
Article Categories:
HistoryTourism