Makumbusho ya Kimondo yafunguliwa Songwe

Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe umefungua Makumbusho ya Kimondo katika kijiji cha Ndolezi katika Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Kimondo cha Mbozi ni moja ya kivutio bora cha utalii katika mkoa wa Songwe na ni miongoni wa vimondo 10 vizito vinavyojulikana duniani na cha pili kwa ukubwa barani Afrika.

Ufunguzi wa Makumbusho ni miongoni mwa hatua za kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza utalii katika mikoa ya Nyanda ya Juu Kusini na pia kuimarisha uhifadhi wa urithi Tanzania wa mila na tamaduni zetu.

Kimondo cha Mbozi kiligunduliwa na Mwafrika aliyejulikana kwa jina la Mzee Halele ambaye alikuwa Mhunzi, hivyo katika harakati zake za kutafuta chuma alikiona kimondo hicho na baadaye kumbukumbu za kimondo hicho ziliwekwa kwenye maandishi na Mzungu aliyeitwa Wiliam Nolt mwaka 1930.

Likes:
0 0
Views:
895
Article Categories:
HistoryTourism