MV Liemba, meli iliyotumika Vita vya Kwanza vya Dunia

Ina jumla ya miaka 109 ambapo ilitengenezwa mwaka 1913 nchini Ujerumani na ikapewa jina la Graf von Goetzen, likiwa ni jina la gavana wa jimbo moja nchini Ujerumani.

Baada ya kutengenezwa ilifunguliwa vipande vipande na kisha kupakiwa kwenye maboksi 5,000 na kusafirishwa kwa meli mpaka Dar es Salaam  Tanzania kisha kusafirishwa mpaka Tabora  na kubebwa na watumwa mpaka Kigoma.

Baada ya kufika Kigoma ikaingizwa kwenye Chelezo na mnamo mwaka 1915 ikaanza kazi rasmi ikiwa na mizinga miwili mbele na nyuma. Pia,  ilikuwa inatumika kusafirisha wanajeshi wa Ujerumani kuwapeleka katika bandari tofauti tofauti kwa ajili ya kupigana vita ikiwa ni pamoja na Bandari ya Kassanga na Mbala iliyopo Zambia.

Mwaka 1916 baada ya ujerumani kuona dalili za kushindwa vita na Muingereza akaamua kuizamisha meli hii kwa makusudi ili Muingereza asiweze kuitumia Meli hiyo, lakini mwaka 1924 Muingereza aliiibua meli hiyo.

Mwaka 1957  ilibadilishwa jina na kuitwa LIEMBA, neno linalotoka kwenye jamii ya Kifipa likiwa na maana ya Maji.

Mwaka 1961 ilikabidhiwa kwa Serikali ya Tanganyika na ikafanyiwa marekebisho yaliyojumuisha kubadilisha mfumo wa injini iliyokuwa inatumika awali ya kutumia mvuke  na kuweka mfumo wa Injini unaotumia dizeli.

Meli hiyo ilikuwa inafanya kazi zake kuzunguka mwambao wa Ziwa Tanganyika ikiwemo Kigoma, Katavi, Rukwa pamoja na nchi jirani ya Zambia na Burundi ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 200 za mizigo

Likes:
0 0
Views:
1255
Article Tags:
Article Categories:
HistoryTourism