Maporomoko ya maji Kalambo

Maporomoko ya maji kalambo yanapatikana kata ya Mpombwe wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.

Ni maporomoko ya pili kwa ukubwa barani Afrika na ya kwanza Afrika mashariki. Yapo mpakani mwa Tanzania na Zambia yakiwa na upana wa mita 3.6 hadi 18 kutegemea na msimu wa mvua.

Ukubwa wake umechagizwa na miingiliano ya maji ya mito mikubwa miwili, Mto Kalambo na Mto Limba pamoja na mito midogo midogo ya misimu.

Huporomosha maji yake bila kugonga miamba kwa zaidi ya asilimia 50 hadi ya tuapo chini ambapo hutengeneza mto mwingine wa maji unaokwenda kumwaga maji hayo katika ziwa Tanganyika baada ya kilomita chache.

Chini ya maporomoko hayo ni Korongo la Kalambo, ambalo lina upana wa takriban kilomita 1.

Likes:
0 0
Views:
639
Article Categories:
Southern Zone