Atengeneza “games” kutangaza vivutio vya Utalii

Mjasiriamali wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Tanzania, Elias Patrick ametengeneza michezo mitatu ya simu kama sehemu ya kuutangaza utalii wa Tanzania kote duniani.

Mtaalamu huyo wa masoko ya kidijitali na uundaji wa tovuti pamoja na programu tumishi, ametengeneza michezo mitatu inayoweza kupakuliwa kwenye simu na yenye majina ya vivutio vitatu vya utalii nchini

Kwa kupitia ‘Kilimanjaro Block Puzzle’, ‘Serengeti Block Puzzle’ na ‘Tanzanite Crush’ ambazo sasa zinapatikana kwenye simu za ‘android’ Patrick amesema “najaribu kurekebisha taarifa za upotoshaji kuhusu ramani sahihi ya baadhi ya maeneo.”

Michezo hiyo ambayo inapatikana katika nchi 172 itawasaidia watalii kujua ukweli wa baadhi ya taarifa za uongo walizolishwa kama ile ya ulipo Mlima Kilimanjaro.

Kwa mwaka 2021 hadi juni 2022 takwimu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha kuwa Tanzania ilipata dola bilioni 1.708 kwenye usafiri katika kutoka dola milioni 871.6 kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Watalii pia waliongezeka kwa 76% hadi kufikia 1,123,607.

Likes:
0 0
Views:
460
Article Categories:
Tourism