Chemchemi ya Maji moto Utete, Rufiji

Chemchemi ya Maji ya moto Utete ipo katika mji wa Utete, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani. Chanzo hicho kipo Mto Rufiji na kati ya misitu ya Utete na Katundu upande wa mashariki na kina ukubwa wa Ekari 2,346 (sawa) na hekta 938.4).

Hifadhi hii ilitengwa na kuanza kuhifadhiwa mwaka 1930 na wakoloni na pia inatumika kama sehemu ya utalii kutokana na uwepo wa chemchemi za maji moto.

Eneo hilo la asili linasimamiwa na Wakala wa Huduma za misitu Tanzania (TFS) na pia wakazi wanaozunguka eneo hilo hulitumia kwa matambiko na shughuli nyingine za kiuchumi.

Hifadhi hiyo ya chemchemi ya maji moto ipo katika msitu wa asili wa Utete na kitundu na pia kuna maeneo mazuri kwa ajili ya ‘picnics’, kukodisha mahema na huduma za usafiri kwa watalii. Shughuli za utalii zinazoweza kufanywa ndani ya hifadhi ni pamoja na:- kupiga kambi, kuangalia chemchemi ya maji moto, kutembea, uvuvi na upigaji picha.

Likes:
0 0
Views:
787
Article Tags:
Article Categories:
Tourism