Dhima ya vyombo vya habari kutangaza utalii

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema vyombo vya habari vina jukumu la kutoa habari, kuelimisha na kutafakarisha umma kupitia vipindi na makala zitazofikisha ujumbe kwa jamii ili kukuza sekta ya utalii nchini.

Dkt. Rioba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika Tamasha la Usiku wa The Royal Tour lililokutanisha viongozi, wadau wa utalii na wasanii lililofanyika mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kuunga mkono sekta ya utalii nchini kupitia filamu ya Tanzania The Roya Tour.

Amesema filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyokuwa ikitazamwa kupitia vyombo vya habari imeleta matokeo chanya katika sekta ya utalii na kutolea mfano wa dereva aliyekuwa akieleza kuwa watalii wengi wanaokuja nchini wanauliza namna watakavyoweza kufika maeneo yaliyoonekana katika filamu hiyo hususani yale ambayo Rais Samia Suluhu Hassani alionekana.

Dkt. Rioba amesema, Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) lilianzisha chaneli ya Utalii -Tanzania Safari Channel ambayo hadi sasa inapatikana katika visimbuzi vyote nchini na channel hii inarusha makala na vipindi vya moja kwa moja vinavyohusu utalii wa ndani ya nchi.

Likes:
0 0
Views:
439
Article Categories:
Tourism