Fahamu historia ya Mnara wa Dkt. Livingstone, Bagamoyo

Agosti 17, 1868 Wamisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu waliwasili Bagamoyo kuanzisha kanisa katoliki. Waliweka alama kwa kupanda Mbuyu na kupandisha msalaba katika eneo la Kisutu, Bagamoyo.

Katika eneo ulipo mbuyu, kanisa la kwanza la katoliki bara (Kanisa Mama ya makanisa yote Katoliki nchini) kwa Afrika Mashariki lilijengwa kuanzia 1868 hadi 1872.

Mei Mosi, 1873, Dkt. David Livingstone alifariki dunia huko Zambia mbapo alipasuliwa na kutolewa moyo na utumbo ambavyo vilizikwa Zambia, huku mwili wake ukipakwa chumvi na kukaushwa kwa wiki mbili kabla ya kuanza safari ya kuupeleka London kwa maziko.

Safari ya kuubeba mwili huo kuupeleka Zanzibar kwa ajili ya kusafirisha kwenda London ilianza na miezi tisa mbele Februari 24, 1874, mwili wa Dkt. Livingstone uliwasili Bagamoyo na kulazwa katika Mnara wa Kanisa Mama kwa usiku mmoja hadi Februari 25.

Mwili huo ulisafirishwa siku hiyo lakini kabla ya kuelekea Zanzibar ulipewa heshima za mwisho chini ya mti uliokuwepo lilipo kanisa la Anglikana, karibu na kanisa mama la katoliki na kisha safari ya kuelekea London ikaanzia pale Zanzibar.

Baada ya miezi 11 tangu kutoka Zambia, hatimaye mwili wa Dkt. Livingstone ulifika London na kuzikwa eneo la Westminster Abbey
Baadaye kanisa liliondolewa lakini Mnara wa kanisa ulibaki na kujulikana kama Mnara wa Dkt. Livingstone.

Likes:
0 0
Views:
1044
Article Categories:
Tourism