Fahamu kuhusu Mnara wa Askari Dar es Salaam

Kwenye televisheni na picha unaonekana kama ni mnara mkubwa sana, ila ukweli ni kwamba historia yake ni kubwa sana kuliko uhalisia wa ukubwa wake. Mnara huo umekuwa karibu na vijana waliokula ujana miaka ya 80 hadi 90, wanahistoria pana kuwa ilikuwa ni ishara ya kufika mji maarufu Tanzania, uwe umeona mnara na kupiga picha, ikiwa umefika Dar es Salaam.

Maarufu kwa jina la “Mnara wa Askari” (Askari Monument or Dar es Salaam African Memorial) ulizinduliwa mwaka wa 1927, uliletwa kutoka nchini Uingereza na mchongaji wa Uingereza James Alexander Stevenson na alisaini sanamu hiyo na jina lake bandia “Myrander”. Kabla ya kutumwa Dar es Salaam, sanamu hiyo ilioneshwa katika Chuo cha Royal, ikipokea sifa kuu.

  • Askari huyo ana bunduki yenye bayonet iliyoelekezwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
  • Sanamu imesimama juu ya msingi wa jiwe.
  • Kwenye pande zake kuna vibao vilivyowekwa wakfu katika Kiswahili (hati ya Kiarabu na Kilatini) na Kiingereza; kwenye pande wa upana kuna vibao viwili vya picha vinavyoonesha wanajeshi wa Kiafrika wanaopigana na kikosi cha wabebaji maandishi ya Kiingereza yanajumuisha “Ukipigania nchi yako hata ukifa wana wako watalikumbuka jina lako.”

Mnara huo wa ukumbusho upo katikati ya mzunguko wa barabara ya Samora Avenue kwenye makutano ya barabara ya maktaba na mtaa wa Azikiwe, mahali panaporipotiwa pia kuwa kitovu cha katikati mwa jiji la Dar es Salaam.

Sanamu la ukumbusho wa askari (askari wa Kiafrika) waliopigana katika vita ya Waingereza dhidi ya Jeshi la Ujerumani katika Afrika Mashariki katika vita ya kwanza ya dunia I.

Sanamu la ukumbusho wa askari limepambwa kwa shaba, linaonesha Askari akiwa amevaa sare ya ya jeshi, ‘bayonet’ ya bunduki yake ikielekeza kwenye bandari iliyo karibu.

Likes:
0 0
Views:
937
Article Categories:
Tourism