Fahamu kuhusu pori la akiba Kijereshi

Pori la Akiba la Kijereshi lililopo wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Kusini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, lilianzishwa mwaka 1994.

Pori hilo ambalo ni njia ya kuhama wanyama pori, kutoka Serengeti na pia ni sehemu ya ikolojia ya hifadhi hiyo, pia nia kimbilio la wanyamapori wakati wa kiangazi na wakati huo huo hulitumia kama eneo la kupumzikia (Buffer Zone) kwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wanyama kama simba, nyati, tembo, impala, nyumbu, mbweha, pundamilia, mbuni, fisi, korongo na swala hupatikana katika eneo hilo ambapo unaweza kufanya utalii wa kupiga kambi na kutembea kwa miguu.

Aidha, katika pori hilo ambalo linafikika kwa njia ya barabara na angani, unaweza kupigapicha kwa ajili ya biashara au filamu na hakuna ada ya kuingia na kamera.

Ukitumka barabara kutoka Lamadi ni mwendo wa kilomita 20, kutoka Bunda ni kilomita 86, kutoka Musoma ni kilomita 137 na kutoka Mwanza ni umbali wa kilomita 135.

Likes:
0 0
Views:
860
Article Tags:
Article Categories:
Tourism