Fahamu kuhusu pori la akiba Mkungunero

Pori la Akiba la Mkungunero ni ukanda wa asili wa wanyamapori wanaohama kutoka Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwenda katika hifadhi za jirani.

Mandhari ya pori hilo yamekuwa kivutio na makazi bora kwa wanyamapori kama vile tembo, nyati, pundamilia, nyumbu na nyati.

Mkungunero ni hifadhi isiyojulikana sana ambayo ni sehemu ya mfumo wa ikolojia wa Tarangire, na kuwa kivutio kwa wageni wanaofanya safari za kitalii katika maeneo hayo.

Pori la Akiba la Mkungunero linapakana katika kanda ya kusini mwa hifadhi ya taifa ya Tarangire iliyopo mkoani Manyara.

Likes:
0 0
Views:
1021
Article Tags:
Article Categories:
Tourism