Gerenuk/Swala Twiga.

Jina Gerenuk ni neno lenye asili ya Ki-somali,likiwa na maana ya Shingo Twiga kwa kiswahili. Gerenuk ni Swala mrembo sana kwa mwonekano akipambwa na mwonekano wa ngozi yake nzuri,shingo ndefu na masikio marefu yanayotoa mwonekano wa herufi Y.

Kama ilivyo kwa jamii nyingi za swala,madume ya Swala Twiga wana pembe wakati majike hawana.

Pamoja na mwonekano mzuri wa kuvutia Gerenuk si katika jamii ya Swala anayefahamika na wengi wetu japo anapatikana hata katika hifadhi zetu hapa Tanzania,sababu ikiwa ni Uchache wao,kwani ni katika moja ya jamii ya Swala ambao wako hatarini kutoweka sababu ikiwa ni uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Ulaji wa Migunga(Acacia) kama moja ya chakula chao kikuu ni sababu nyingine inayowafanya wao kufananishwa na Twiga achilia urefu Wa shingo zao.

Mara nyingi wakati wa kula Gerenuk huonekana wakiwa wamesimama na miguu yao ya nyuma huku wakila kwenye matawi ya miti ya migunga na ni adimu sana wao kuonekana wanakula majani yaliyo chini yani kama ilivyo adimu kumuona Twiga anakula majani ya chini basi na Gerenuk ni hivyohivyo.

Swala Twiga huyu(jike) alionekana katika shamba la hifadhi ya wanyama ya Chato.

Likes:
0 0
Views:
65
Article Categories:
Tourism