Hifadhi ya Msitu ya safu ya milima ya Udzungwa

Hifadhi ya Misitu ya Safu ya Milima ya Udzungwa (USNFR) ina ukubwa wa hekta 32,763.2 na urefu wa mpaka wa takriban kilomita 126. Inapatikana katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania ndani ya katika wa Iringa na mkoani Morogoro.

Kwa Mkoa wa Iringa Hifadhi hiyo iko ndani ya wilaya za Kilolo na Mufindi na katika mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilombero.

Hifadhi hiyo ya Milima ya Udzungwa, ni sehemu ya mlolongo wa Milima ya Tao la Mashariki.

USNFR inajumuisha misitu mirefu ya kifahari ya nyanda za juu na misitu midogo midogo. Mimea iliyopo ndani ya safau ya milima hiyo ya Tao la Mashariki ni ile inayotumiwa katika tafiti na baadhi ya nchi ulimwenguni.

Kuna njia kuu tatu za kufika katika hifadhi hiyo:- Kwanza ni kupitia Ipogoro, Wilaya ya Kilolo ambayo ni takriban kilomita 80 hadi 100 kutoka Iringa Mjini.

Njia ya pili ni kupitia Wilaya ya Mufindi takriban kilomita 130 kutoka mji wa Mafinga mkoani Iringa, huku njia ya tatu ni kupitia Mikumi mjini kupitia Ifakara hadi Itongoa ambayo ni takriban kilomita 80 kutoka Ifakara mjini.

Vivutio vya utalii ni pamoja na; Uzungwa escarpment, Colobus monkeys( red and black white ) water falls (Idasi, Funo and Ilutila ) Natural dams(Mkololo ),chura anayepanda miti (Hyperolius kihangensis), mikunjo (Ilutila,Ngwilo).

Likes:
0 0
Views:
51
Article Categories:
Tourism