Hifadhi ya Taifa Mikumi

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro ni mbuga rahisi kufikika. Itakuchukua takribani saa 1 kutoka Morogoro Mjini hadi geti kuu la hifadhi hiyo yenye sifa kubwa ya kuwa na wanyama wengi na wanaoweza kuonekana kwa urahisi.

Aidha, Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ni mbuga ambayo unaweza kutembelea wakati wote na ukiwa njiani pia unaweza kushuhudia wanyama mbalimbali pembezoni mwa barabara.

Ukiwa unaelekea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi unaweza kufanya utalii milima ya uluguru mpaka kwa Kingalu Mwanabazi na pia ukiwa njiani unaweza tembelea Maasai Village Melela na kula nyama choma

Watalii wengi hupenda kutembelea Mikumi kutokana kuwa na hali ya hewa nzuri na huduma za malazi zikiwa karibu na hifadhi hiyo yaani mji wa Mikumi na Morogoro Mjini.

Likes:
0 0
Views:
25
Article Tags:
Article Categories:
Tourism