Ifahamu hifadhi ya mazingira asilia mlima Rungwe

Hifadhi ya Mazingira Asilia Mlima Rungwe ni hifadhi inayopatikana katika Wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya ikiwa na ukubwa wa hekta 24,680.5.

Hifadhi hii ipo umbali wa takribani kilometa 25 Kusini Mashariki mwa mji wa Mbeya na umbali wa 7km Kaskazini mwa mji wa Tukuyu.

Hifadhi Asilia ya Mlima Rungwe ni ya kipekee kwa kuwa na uoto aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na msitu wa mlimani (lower and upper montane forests), ukanda wa mianzi (bamboo belt), heathland, mchanganyiko wa miti mifupi na nyasi (woodland), na nyasi (grassland).

Ni sehemu ambayo sampuli ya nyani anayepatikana Tanzania pekee (Rungwecebus Kipunji) ilichukuliwa na hivyo nyani kupewa jina la Rungwe kama sehemu ya ukumbusho.

Ni Mlima wa tatu kwa urefu Tanzania ukiwa na urefu wa meta 2,981 baada ya Kilimanjaro (5,595m) na Meru (4,600m).

Ni sehemu inayopokea mvua nyingi kuliko sehemu yoyote nchini ikiwa inapata mvua yenye ujazo mm 3,000 kwa mwaka.

Mbali na hivyo Wanyama wadogo wadogo zaidi ya zaidi ya aina 500 kama vile Minde (Abbot duiker), chura wekundu, mijus, nyoka wa nchi baridi, panya hupatikana. Pia, zaidi ya aina 400 za mimea hupatikana ambapo baadhi ya mimea hiyo hutumika kama dawa kwa wakaazi waliozunguka hifadhi hiyo.

Likes:
0 0
Views:
775
Article Categories:
Tourism