Kampuni za ulinzi zaunga mkoani The Royal Tour

Kampuni binafsi za ulinzi mkoani Arusha zimeahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kutangaza sifa njema ya Tanzania na kuvutia wageni kwa kutoa ulinzi kwenye hoteli wanazofikia watalii.

Aidha, kampuni hizo zimeahidi kuwa katika kufanya kazi hiyo zitashirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha usalama wa wageni na mali zao katika muda wote wanapokuwa mkoani humo.

Wametoa ahadi hiyo wakizungumza na Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi Joswamu Kaijanante ambaye amewaambia kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kwa ujio mkubwa wa wageni baada ya uzinduzi wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Likes:
0 0
Views:
35
Article Categories:
Tourism