Kereng’ende, mdudu anayeashiria ubora wa makazi

Kereng’ende ni wadudu wa kawaida ambao mara nyingi hupatikana karibu na maeneo yenye maji baridi. Kereng’ende ni viashiria vya ubora wa makazi ya majini na nchi kavu.

Kereng’ende ni wadudu walao nyama na wanaowinda wadudu wengine, kama vile mbu na nzi. Wana macho makubwa na antena fupi. Wadudu hawa wamejengeka kwa nguvu zaidi na wanaruka haraka kwa kasi ya hadi kilomita 56 kwa saa na huruka kinyumenyume, vile vile kwa kunyanyuka wima, mtindo wa helikopta. Wakiwa wamepumzika, hushikilia mbawa zao wima.

Mayai hutagwa kwenye miti ya kijani kibichi au vichaka vinavyoning’inia juu ya maji, maisha yao ya vibuu yapo kwenye makazi ya majini na akiwa imago hutumia anuwai ya makazi ya nchi kavu. Unyeti wao katika ubora wa makazi ya asili huwafanya kuwa viashiria muhimu vya ubora wa makazi, juu na chini ya uso wa maji. Uchaguzi wa makazi ya kereng’ende wakubwa unategemea sana muundo wa mimea, ikiwa ni pamoja na uwepo kivuli.

Unaweza kuwatazama vyema wadudu hawa wazuri katika maeneo mbalimbali yenye vyanzo vya maji safi.

Likes:
0 0
Views:
832
Article Tags:
Article Categories:
Tourism