Mfahamu Korongo Mfuko Shingo (Marabou Stork)

Wengine wanamuita Ndege joni. Ni ndege mkubwa ambaye anakula  vyakula vya aina mbalimbali kama mizoga, wadudu, nyoka, panya, samaki, vyura, ndege na viumbe wengine wengi. 

Ndege hawa wana miguu mirefu yenye ngozi ambayo huwasaidia kupenyeza kwenye maji pale  inapobidi na mdomo mkubwa wa manjano iliyokolea.Wana macho madogo yaliyozungukwa na ngozi tupu yenye madoadoa mekundu. 

Ndege Joni ana mfuko mrefu, mwekundu unaoning’inia shingoni mwake. Kifuko hiki hufikia urefu wa inchi 18 na hutumika  hasa katika  msimu wa kuzaliana ambapo hutumika kumvutia Mwenza. 

Makala muhusu Korongo Mfuko Shingo anayepatikana katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo itakujia hivi karibuni kupitia TANZANIA SAFARI CHANNEL.

Likes:
0 0
Views:
996
Article Categories:
Tourism