Mlima Mwalolera au kama unavyofahamika pia kama Mlima Bulera unapatikana katika maeneo yenye uoto wa asili katika mkoa wa Geita.
Hapa kuna alama mbalimbali za kihistoria vikiwemo visima vitatu vilivyokuwa kwenye miamba ya mawe katika mlima huu, ambapo visima hivyo vilitumika kama vyanzo vikuu vya maji kwa wakazi wa jirani na mlima huu.
Visima hivyo vilikuwa na maajabu yake kwani ilikuwa ni mwiko kwa mtu mwenye kitovu kikubwa kusogelea, pia ilitakiwa kusogea maeneo hayo ukiwa peku, na mama mwenye watoto pacha hakutakiwa kabisa maeneo hayo.