Polisi Arusha waja kivingine ongezeko la watalii

Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua filamu ya Tanzania: The Royal Tour inayovutia watalii wengi kuja kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii Tanzania, Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha usalama wa watalii na mali zao.

Kwa niaba ya msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema jeshi la polisi limeanzisha kitengo maalum cha Utalii na Diplomasia kwa ajili ya kuwahudumia watalii na wanadiplomasia wanaofiika nchini kutalii ama kuwekeza.

Jiji la Arusha ndio kitovu cha utalii nchini na kikosi hicho ambacho kimepatiwa mafunzo ndani na nje ya nchi juu ya namna bora ya kuhudumia watalii kimefunguliwa kituo rasmi mkoani hapo. Sambamba na vituo vidogo vya polisi wilayani Arumeru, Karatu, Monduli na Longido vitavyotumika kutoa taarifa za kitalii na ukaguzi wa magari ya kitalii

Aidha, ACP Masejo amesema kuwa kuna magari maalum ya doria katika maeneo mbalimbali ya Arusha ikiwemo kwenye vivutio vya utalii, hoteli za kitalii pamoja na maeneo mengine ambayo wageni hupenda kutembelea.

Likes:
0 0
Views:
239
Article Tags:
Article Categories:
Tourism