Sababu 5 za kutembelea Pori la Akiba la Selous

Pori la Akiba la Selous ni mojawapo ya hifadhi kubwa zaidi za wanyamapori hapa nchini.

Pori hili lipo Kusini mwa Tanzania.

Hizi ni sababu 5 kwanini utembelee Seluos;

  1. Safari za kutembea (Walking Safaris) kwa kuongozwa ni njia nzuri za kiasili zitakufanya ufurahie mandhari nzuri ya pori hilo huku ukipata fursa ya kujionea uoto wa asili, wanyama na ikolojia ya maeneo mbalimbali ya hifadhi.
  2. SAFARI YA BOTI:

Utapata uzoefu wa kutalii na kujionea fahari ya maeneo yanayozunguka mto rufiji ndani ya hifadhi ya Selous.

Furahia safari chini ya Mto Rufiji mkubwa au mojawapo ya vijito vyake ambapo wageni wanaona mamba na viboko wengi pamoja na aina mbalimbali za ndege.

Wanyama wengine wenye kiu mara nyingi wanaweza kuonekana karibu.

  1. UVUVI

Uvuvi wa Samaki wa maji baridi ambao utakupa fursa ya kuvua samaki na kuwaachia hasa nyakati za jioni utakufanya kufurahia jioni tulivu kwenye kingo za mto Rufiji.

  1. UTALII WA MAGARI

Ukiwa Selous unaweza kufanya utalii kwa kutumia magari maalumu na kitalii kujionea vivutio vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo.

Utawaona wanyama wa aina mbalimbali kama Simba, Mbwa mwitu, Tembo na makundi makubwa ya nyati.

  1. NDEGE

Selous ina aina kubwa ya ndege na zaidi ya spishi 400 zilizorekodiwa.

Ndege kadhaa wanaohama kutoka Ulaya na Afrika Kaskazini wanaweza kuonekana hasa kati ya Novemba hadi Machi.

Likes:
0 0
Views:
696
Article Tags:
Article Categories:
Tourism