The Royal Tour yamleta Mwekezaji Mkubwa wa Marekani

Jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii nchini kupitia Filamu ya Tanzania: The Royal Tour zinaendelea kuzaa matunda nchini.

Licha ya kupokea watalii wengi, Mwekezaji Mkubwa wa hoteli za Kifahari nchini Marekani, Munir Walji amewasili nchini kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana kuhusu uwekezaji wa hoteli za kitalii ambazo zitaongeza thamani katika sekta ya hiyo ili kwenda na kasi ya ujio wa watalii wengi.

Katika mazungumzo yao Dkt. Chana amemshukuru na kumpongeza Walji kwa uamuzi wa kutaka kuwekeza katika sekta ya utalii hapa nchini na kumwahidi kumpa ushirikiano mkubwa ili aweze kufanikisha azma yake njema kwa Tanzania.

Naye Walji ameipongeza Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri yanayohamasisha na kuvutia wawekezaji katika sekta ya utalii pamoja na kuvitangaza vyema vivutio vya Utalii hali inayoongeza idadi ya watalii.

Aidha, mwekezaji huyo amesema kuwa ameona ipo haja ya kuchangamkia fursa kwa kuwekeza kwenye sekta ya Utalii hapa nchini.

Likes:
0 0
Views:
473
Article Categories:
Tourism