Ufumbuzi wapatikana tatizo la wanyama wakali na waharibifu

Vituo vya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu wanaovamia makazi ya watu na kuharibu mali, mazao, mifugo na hata kujeruhi vinaendelea kujengwa ili kuwaepusha wananchi na majanga hayo.

Vituo 16 vitavyokuwa na askiri saa 24 vimeanza kujengwa nchi nzima karibu na maeneo ya wananchi ikiwemo katika Pori la Akiba Nkungunero wilayani Kondoa, Dodoma kufuatia agizo la Waziri Mkuu wakati wa Bunge la Bajeti 2022 ili kutatua matatizo hayo kwa haraka na kuepusha athari zinazoepukika.

Hivyo agizo hilo ni kufuatia malalamiko ya wananchi waishio karibu na maeneo ya hifadhi na mapori yaliyowasilishwa na wabunge wao bungeni.

Sehemu zilizonufaika na ujenzi huu ni pamoja na Mtera, Ilangali, Mwanga, Iringa, Tabora na nyingine nyingi.

Mwanzoni mwa mwezi huu Serikali ya Tanzania, ilipokea Euro milioni sita sawa ba bilioni 13.2 kutoka Shirika la Ujerumani la GIZ, kusaidia kupunguza migogoro ya wananchi na wanyamapori kwenye maeneo ya pembezoni mwa hifadhi.

Likes:
0 0
Views:
474
Article Tags:
Article Categories:
Tourism