Utalii katika Hifadhi ya Taifa Milima Mahale

Ni hifadhi iliyopo mkoa wa Kigoma wilaya ya uvinza, ambapo unaweza kufika kwenye hifadhi hii kwa kutumia Usafiri wa gari (barabara) , usafiri wa ndege (Anga) pamoja na usafiri wa Boti kufika katika hifadhi hii.

Katika hifadhi hii kuna vivutio vya kitalii vya aina mbalimbali ikiwemo utalii wa kuangalia ndege ambao wanapatikana pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Wanyamapori mbalimbali wanapatikanaa katika hifadhi hii ikiwemo wanyama aina ya pongo –(bushback) pamoja na sokwe ambao kwa ujumla wanaleta kivutio kizuri cha utalii.

Pia katika hifadhi hii unaweza kufanya utalii wa kupiga makasia (Kayaking) katika ziwa Tanganyika ambalo lina urefu wa kilometa za maraba 673 kutoka kaskazini hadi kusini Na linatumika kama kiunganishi cha maeneo mbali mbali katika hifadhi hii.

Hifadhi hii imejumuisha maeneo mbali mbali ya Muinuko ambapo muinuko mkubwa zaidi katika mkoa wa kigoma unapatikana katika hifadhi hii pamoja na maeneo mengine ya miinuko ambayo huvutia watalii wengi kupanda katika Kilele cha Nkungwe ambacho kina mita 2462 kutoka usawa wa bahari.

Utalii wa kuvua samaki


Ukarimu wa waongoza watalii pia inafanya hifadhi hii kuwa rafiki kwa kila mgeni anayekuja kufanya utalii katika hifadhi.

Likes:
0 0
Views:
537
Article Tags:
Article Categories:
Tourism