Utalii wa baiskeli kuutangaza Mlima Kilimanjaro

Watanzania walioungana na waendesha baiskeli duniani,  akiwemo mwendesha baiskeli nguli kutoka Uingereza Hannah Barnes, wamesafiri kilomita 275 kupitia Mlima Kilimanjaro hadi Ziwa Natron kwa muda wa siku nne ili kuutangaza utalii wa baiskeli katika mlima huo.

Akizungumza mara baada ya kumaliza safari hiyo Miss Utalii Njombe, Zawadi Mwambi amesema kwake imekuwa ni faraja kuendelea kushirikiana na waendesha baiskeli duniani katika kuutangaza utalii wa Tanzania, hasa Mlima Kilimanjaro ambao kwa miaka mingi wengi wamekuwa wakipotoshwa na sehemu mlima huo ulipo.

Mwendesha baiskeli kutoka Uingereza, Hannah Barnes amesema amevutiwa sana na hali ya hewa ya mlima na imekuwa ni rafiki kwa waendesha baiskeli kumaliza safari yao salama.

Waendesha baiskeli kutoka Tanzania wamekuwa mstari wa mbele katika kuendelea kuvitangaza vivutio kwa utalii nchini wakiwa katika misafara yao mikubwa kama vile Twende Butiama safari ambayo inawachukua siku 10 kusafiri kilomita 1500 kutoka Dar es Salaam hadi Mwitongo, Butiama mkoani Mara.

Likes:
0 0
Views:
581
Article Categories:
Tourism