Utalii wa kupanda farasi Iringa – Tanzania

Utalii wa kupanda farasi ni mojawapo ya utalii ambao mtu hupanda farasi na kuzunguka maeneo mbalimbali kujionea mandhari na vivutio vya kitalii.

Farasi hao wana majina na hutembezwa kwa mwendo tofauti kulingana na uzoefu na mahitaji ya mtalii ambapo kama mtalii si mzoefu farasi atapelekwa kwa mwendo wa pole pole na kwa wazoefu farasi hukimbizwa kwa mwendo wa haraka.

Utalii huu upo mkoani Iringa wilayani Mufindi katika kijiji cha Luhunga ambapo watalii hutembelea eneo hilo lenye mandhari nzuri lililozungukwa na milima hivyo kuwa na muonekano mzuri na hewa nzuri jambo linalofanya watalii kutembea na Farasi eneo kubwa na kujionea mandhari zaidi.

Likes:
0 0
Views:
846
Article Categories:
Tourism