Wataalamu wa malikale wakutana Arusha

Wataalam wa Fani ya Malikale wa Tanzania na Kimataifa wametakiwa waendelee kufanya tafiti zaidi nchini Tanzania kuibua maeneo zaidi yenye Urithi wa Masalia ya Kale ili jamii iweze kunufaika na matokeo ya tafiti zao.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa wataalam wa Fani ya Masalia ya Kale, Jijini Arusha.

Dkt. Chana amesema matokeo Chanya ya kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuibeba sekta ya Utalii kupitia Filamu ya The Royal Tour, yawe kichocheo cha ongezeko la tafiti zitakazo ibua maeneo mapya ambayo yatavutia watalii zaidi.

Nchi zaidi ya 15 zinahudhuria mkutano huo, zikiwemo, Marekani, Canada, Uingereza, Ujerumani, Hispania, Italia, Uswisi, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, India, Afrika Kusini, Ethiopia, Kenya ,Tanzania na Uganda.

Kufanyika Kwa mkutano huo nchini Tanzania kunatoa fursa kwa watalaam hao kutembelea maeneo mbalimbali yenye historia kubwa ya Masalia ya Kale likiwemo eneo la Olduvai Gorge na Laetoli ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Likes:
0 0
Views:
397
Article Tags:
Article Categories:
Tourism