Watalii 26 kutoka mikoa mitatu wafanya Utalii shamba la miti Ukaguru

Watalii 26 kutoka katika mikoa mitatu wametembelea shamba la miti la Ukaguru lililopo mkoani Morogoro.

Lengo kuu  la kufanya utalii huo ni kutangaza vivutio vilivyopo ndani ya Shamba hilo.

Watalii hao ni kutoka Mikoa ya Morogoro, Dar es Salam na Dodoma ambapo walikuwepo pia watoto waliofika katika shamba hilo kwa lengo la kukifunza.

Uongozi wa Shamba hilo linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Kanda ya Mashariki ulipokea  Watalii 20 kutoka kituo Cha watoto Tumaini Foundation kilichopo Dodoma, wanne kutoka Wilaya ya Gairo, Dar es Salaam na mmoja Morogoro.

Watalii hao wamefanya utalii huo katika kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuunga mkono  Utalii wa ndani kupitia Filamu ya Tanzania The Royal Tour iliyozinduliwa hivi karibuni,ili kuleta tija katika mnyororo wa thamani katika Utalii nchini. 

Likes:
0 0
Views:
389
Article Tags:
Article Categories:
Tourism