Watalii wamiminika katika Hifadhi ya Ziwa Manyara

Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii baada ya Brazil. Maelfu ya Watalii huja nchini kila mwaka ambapo hutembelea vivutio hivyo kuanzia fukwe, hifadhi za wanyama, maeneo ya kiutamaduni na kihistoria.

Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara hupokea wageni wengi ambao huichagua kutokana na urahisi wa kuona wanyama mbalimbali kama vile Tembo, Simba, Twiga, Chui na wengine wengi.

Pichani ni baadhi ya watalii wakimtazama Tembo aliyefunga njia wakati wakiendelea na shughuli za kitalii. Ujio wa watalii hao umechangiwa pia na filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo imeitangaza Tanzania na vivutio vyake.

Likes:
0 0
Views:
651
Article Tags:
Article Categories:
Tourism