Waziri Dkt. Pindi Chana ahimiza upandaji miti

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa jamii kupanda miti kwa kuwa upo uhitaji mkubwa wa bidhaa zinazotokana na misitu ndani na nje ya Tanzania.

Aidha, ameeleza kuwa miti ni fursa muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja naTaifa kwa aujumla.

Dkt. Chana ameyasema hayo alipotembelea Shamba la Miti la Sao Hill, Kiwanda cha Lush Chanzo kinachotengeneza bidhaa mbadala ya mbao (MDF), pamoja na Mradi wa Maendeleo Endelevu ya Misitu (FDT), wilayani Mafinga mkoa wa Iringa.

Waziri Dkt.Pindi Chana licha ya kuwapongeza wadau wa Maliasili na Utalii kwa uwekezaji mkubwa kwenye misitu na uchakataji wa Mazao ya Misitu, amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ili kuiendeleza sekta hiyo hapa nchini.

Akielezea hatua mbalimbali za uhifadhi wa Misitu Mhifadhi Mkuu wa Shamba Miti la Sao Hill Lucas Sabida amesema licha ya kuwa na Shamba kubwa la miti waneendelea kuotesha miche zaidi ya miti, kuelimisha na kuishirikisha jamii katika kuhakikisha inaongeza umiliki wa mashamba ya Miti.

Likes:
0 0
Views:
261
Article Tags:
Article Categories:
Tourism