Yafahamu matunda ya filamu ya Tanzania: The Royal Your

Tarehe 18 Aprili 2022, Tanzania iliweka alama isiyofutika katika historia ya nchi kupitia uzinduzi, kwa mara ya kwanza New York nchini Marekani, wa filamu iliyolenga kufungua fursa za kitalii, uwekezaji na biashara kwa kiionesha dunia vivutio vyake ambavyo vinaipa nchi upekee na kuifanya tofauti na nchi zingine.

Hivi karibuni Tanzania na Marekani  zimesaini  mikataba ya kiitifaki yenye lengo la kuboresha usafiri wa anga. Si jambo geni kusikia nchi hizi mbili zimesaini mikataba, ila ni jambo la kipekee kusikia aina ya mkataba uliosainiwa hivi karibuni utakao ziwezesha nchi hizi kushirikiana vyema katika usafiri wa anga.

Kwa kuzingatia mkataba uliosainiwa hivi karibuni wenye lengo la kuboresha usafiri wa anga, ikiwa ni kwa maana ya kufungua soko la ndege za abiria na mizigo ambapo ndege hizi zitakuwa zikiruka moja kwa moja kutoka Marekani hadi Tanzania. Kama nchi unaweza jiuliza hili linamanufaa gani?

Mosi, katika sekta ya utalii huduma hii inakwenda kurahisisha usafiri kwa watalii pamoja na wawekezaji kutoka nchini Marekani. Ikumbukwe awali usafiri kutoka marekani hadi Tanzania ulikuwepo ila sio wa moja kwa moja, ilimuhitaji mtalii au mwekezaji kuunganisha ndege au kuwa na vituo vingi njiani vya kupumzika ili kupisha ndege kupakiza na kushusha abiria katika nchi baadhi.

Pili, baada ya usafiri kurahisishwa hili linakwenda kuchangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la watalii na wawekezaji kwani urahisi huu utaibua hisia za watalii kushawishika kuwa na mipango ya kuitembekea Tanzania. Ikumbukwe jambo linapokuwa jepesi basi kila mmoja huwaza kufaidi wepesi huo.

Tatu, kiwango cha watu kusafiri, kufanya biashara na uwekezaji kitaongezeka kutokana na mazingira rafiki. Hili linakwenda kuongeza fursa za ajira nchini hususani ajira katika sekta ya utalii, uwekezaji na biashara.

Wengi wangejiuliza fursa zote hizi zilikuwa wapi kabla, ila kuna msemo wa waswahili usemao ‘Mkaa bure sio sawa na mtembea bure.’ Kwa kuona manufaa yote haya ni dhahiri kuwa haya ni matunda ya filamu ya Tanzania: The Royal Tour. Tuwe tayari, yajayo yanazidi kufurahisha.

Likes:
0 0
Views:
507
Article Tags:
Article Categories:
Tourism