Zifahamu tabia za Mamba

Kando ya mto Wami, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani, wamejipanga viboko na Mamba wanaotumia muda huo kuota jua.

Pichani ni mamba akiwa amejilaza mdomo wazi. Wakati anaota jua mamba huweza kuuacha mdomo wake wazi kwa dakika 10 hadi 15.

Wengi hudhani kuwa tabia hiyo ya mamba ni kwa ajili ya kuwinda wadudu, lakini Mamba hufanya hivyo ili kusafisha kinywa chake.

Anapofungua mdomo, hutoa harufu yenye kusambaa umbali wa mita 200 hadi 400 na kuvutia ndege wajulikanao kama ‘Plovers’ ambao huja na kuingia kinywani mwa mambo kumsafisha kinywa kwa kula uchafu uliopo kinywani mwake.

Mamba anauwezo wa kukaa nje ya bahari kwa dakika 45 hadi saa nzima kabla ya kurudi ndani ya maji na kukaa kwa saa kadhaa kabla ya kutoka tena nje.

Katika eneo hilo chakula chao kikubwa ni viumbe vingine vya majini. Na anapokula akashiba, mamba hutoka nje na kula mawe madogo madogo yanayoenda kusaidia kwenye kumeng’enya chakula (digestion).

Endapo ukashambuliwa na mamba, inashauriwa kutumia vidole vyako viwili na kuviingiza ndani ya pua zake ama machoni ili kujiokoa. Kitendo hicho humfanya mamba akuachie mara moja.

Likes:
0 0
Views:
839
Article Tags:
Article Categories:
Tourism