Ziwa Rukwa, ziwa linaloongezeka ukubwa kila siku

Ziwa Rukwa ni moja kati ya maziwa yenye asili ya maji ya magadi nchini Tanzania. Ni moja ya maziwa ambayo hupokea maji kutoka vyanzo vingine vya maji ila lenyewe haliyatoi maji hayo.

Takribani asilimia 80 ya eneo la Pori la Akiba Uwanda ni eneo la Ziwa Rukwa.

Pori la hilo lipo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania na limegawanyika katika sehemu kuu mbili nazo ni sehemu ya maji ambayo huunda Ziwa Rukwa na sehemu ya nchi kavu, ambapo sehemu ya maji ni kubwa zaidi kuliko nchi kavu.

Pori la Akiba la Uwanda lilianzishwa mwaka 1974 na lina ukubwa wa kilomita za mraba takribani 5,000.

Ziwa Rukwa ni kivutio cha kipekee katika Pori la Uwanda kwanu kupokea kwake maji bila kuyatoa kunasababisha kuendelea kuongezeka ukubwa wa ujazo wake kila baada ya kipindi fulani.

Ziwa hilo limezingirwa na safu za milima ya Liembalyamfipa iliyofunikwa na msitu mnene wenye mandhari nzuri ya kuvutia na mito mikubwa na midogo inayopeleka maji moja kwa moja katika ziwa hilo.

Maji yake ni ya magadi na huvutia aina ya ndege wafahamikao kama Lesar Flamingo. Ndege hao huhama kutoka eneo moja kwensa jingine na hufika kwenye ziwa kama sehemu ya malisho zaidi kuliko mazalia.

Uwapo ziwani hapo utapata fursa ya kuona aina mbaimbali za ndege, samaki na wanyama kama vile Kiboko.

Likes:
0 0
Views:
16
Article Tags:
Article Categories:
Tourism