Gangilonga, Jiwe linalosema

Gangilonga ni muunganiko wa maneno mawili ya kihehe ambayo ni Iliganga lyelilonga ambapo Liganga inamaana ya Jiwe na Lilonga ikimaanisha lisemalo hivyo maana yake ni jiwe linalosema.

Kuna maelezo ya aina mbili kuhusu tafsiri ya jiwe Gangilonga. Moja inasema mwamba huu ulitumiwa na wahehe kama mahali kwa ajili ya matambiko na kuongea na mizimu.

Nyingine inaeleza kuwa wakati wa vita vya msituni kati ya mwaka 1894 hadi 1898 Chief Mkwawa aliona kuwa Gangilonga panafaa kufatilia nyendo na shughuli za wajerumani Iringa Mjini kwakuwa ukiwa juu ya jiwe hilo unaiona Iringa vizuri zaidi.

Maskauti wa Mkwawa waliigiza milio ya ndege kwa lengo la kupeleka taarifa muhimu kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa umbali mrefu.

Ukiwa juu ya jiwe hilo watu wanaweza kufanya hata sherehe ya watu Mia moja kutokana na upana wake.

Watu wengi hupenda kutembelea jiwe hilo na kupanda juu kwani kuna mazingira mazuri hivyo hupumzika na wengine hupendelea kwenda kuomba kutokana na imani zao.

Likes:
0 0
Views:
755
Article Categories:
Uncategorized