Huyu ndiye southern ground hornbill

Mumbi Kusi (Southern Ground Hornbill) ni jamii ya Hondohondo wanaopatikana katika hifadhi ya pori la akiba Rungwa.

Mara nyingi ndege hawa huonekana wakitembea ardhini huku wakitumia muda kidogo kupaa kuelekea matawi ya miti jirani, tabia hii ya kutembea zaidi kiliko kupaa ina chagizwa na uzito wao mkubwa unaowalazimu kutumia nguvu nyingi sana kukaa angani/kupaa.

Ingawa Mumbi Kusi hula mbegu,matunda na wadudu, wana uwezo pia wa kuwinda mijusi na viumbe wengine wadogo.

Mumbi Kusi (Southern Ground Hornbills) ndiyo Hondohondo wakubwa zaidi duniani.

Tanzania Safari Channel# Utalii # Itigi # Rungwa # Manyoni # Singida