Matumizi ya maji chemchemi ya Asili Kondoa

Katikati ya Kondoa Mji ipo chemchem ya maji inayozungukwa na madhari nzuri ya misitu na viumbe hai mbalimbali wakiwemo ngedere, nyoka na chui mmoja.

Chemchemi hiyo yenye maji asili ya chumvi imejengewa ukuta na kuifanya iwe chanzo cha maji kikubwa chenye uwezo wa kusambaza maji kwa wakazi wa eneo hilo.

Wageni pia husafiri kutoka sehemu mbalimbali hata Zanzibar huja kuchukua maji haya ambayo huyatumia kuondoa balaa na kuponya magonjwa.

Chemchemi hii inasemwa kuwa ndiyo chanzo kikuu cha maji yanayotumiwa na wakazi wa eneo hilo kwa 85%.

Likes:
0 0
Views:
610
Article Tags:
Article Categories:
Uncategorized