Mlo wa Ugali, fahari ya Afrika

Fahamu hii, mwaka 2017 Ugali uliongezwa kwenye orodha ya UNESCO “Representative List of the Intangible Cultural Heritage of Humanity,” kama mlo maarufu sana bara la Afrika na wenye kuunganisha tamaduni ya vyakula vya Afrika ukiwa mojawapo ya vyakula vichache kwenye orodha hiyo.

Ugali ni aina ya uji wa unga wa mahindi mgumu unaotengenezwa barani Afrika hasa Tanzania. Cha kuvutia zaidi Ugali unajulikana kwa majina mengi kama vile vuswa, bogobe, fufu, gauli, gima, isitshwala, kimnyet, kuon, mieliepap, ngima, nshima, obokima, obuchima, obusuma, oshifima, oruhere, pap, phutu, posho, sadza, ubugali, umutsima, na majina mengine.

Wakati mwingine Nsima ambayo pishi lake linaendana na ugali hutengenezwa kwa unga mwingine, kama vile unga wa mtama au viazi lishe na wakati mwingine huchanganywa na unga wa muhogo.

Ugali unapikwa kwa maji yanayochemka, maziwa au tui la nazi kisha unga husongwa hadi kufikia uthabiti mgumu, kuiva na kuliwa kutegemea na kabila husika. Mfano, Wambulu hupika ugali “kwante” mlaini ambao sio mgumu, wa wastani ya ugali uliyozoeleka na makabila mengine Tanzania.

Sifa ya pili ya mlo wa ugali kwa utamaduni wa sasa nni kuliwa na mboga mboga “mboga saba” na maziwa ya mgando.

Je! Kwenu ugali lazima uwe na sifa gani?

utaliiwachakula #foodtourism

Likes:
0 0
Views:
696
Article Categories:
Uncategorized