DC ataka kutangazwa vivutio vya utalii Sumbawanga

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Sebastian Waryuba ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo wilayani humo, ili viweze kutambulika kwa wenyeji pamoja na wageni kutoka mataifa mbalimbali.
 
Waryuba ametoa wito huo alipokutana na baadhi ya Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa lengo la kujadili namna ya kuvitangaza na kuviendeleza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo wilayani Sumbawanga.


 
Watumishi hao wa TBC wapo wilayani Sumbawanga kwa ajili ya kutayarisha makala zitakazoelezea vivutio vya utalii vilivyopo wilayani Sumbawanga ambavyo vitakuwa vikitangazwa katika chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari.
 
Wakiwa wilayani Sumbawanga, Watumishi hao wa TBC watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwa ni pamoja na msitu wa Mbizi, Pori la akiba la Uwanda, Bwawa la Kwela, bonde la ziwa Rukwa pamoja na kujionea  utamaduni wa maisha ya watu wa Sumbawanga.

Likes:
0 0
Views:
1182
Article Categories:
CaltureWildlife