Idadi ya tembo yazidi kuongezeka

Kwa mujibu wa waziri ya Maliasili na Utalii, Tanzania idadi ya tembo nchini imeendelea kuongezeka kutokana na udhibiti na kupungua kwa ujangili

“Jitihada hizo zinadhihirishwa na matokeo ya sensa ya wanyamapori iliyofanyika mwaka 2021 ambapo idadi ya tembo imeongezeka kwa asilimia 30 katika Mfumo Ikolojia Ziwa Natron – West Kilimanjaro.” amesema Waziri Balozi Pindi Chana

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana amesema takwimu hizo leo 3/06/2022 wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023

Aidha, Waziri Chana amesema pia katika mfumo Ikolojia Ruaha – Rungwa pia idadi ya nyati imeongezeka kwa asilimia 80, pundamilia asilimia 36, idadi ya faru weusi ambao wako hatarini kutoweka imeongezeka kwa asilimia 27.5 na palahala asilimia 65 ikilinganishwa na sensa iliyofanyika mwaka 2018

“Ongezeko la wanyamapori hao ni kiashiria cha kuimarika kwa ulinzi na usimamizi wa maeneo ya hifadhi”amesema Waziri Balozi Pindi Chana

Utafiti huwo upo chini ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori – TAWIRI ambayo ina jukumu la kuratibu na kufanya tafiti za wanyamapori nchini ambapo katika kutekeleza jukumu hilo, Taasisi hiyo inakusanya idadi ya wanyamapori

Likes:
0 0
Views:
777
Article Categories:
TourismWildlife