Ifahamu Hifadhi ya Taifa Gombe

Hifadhi ya Taifa Gombe ni hifadhi ya pili kwa udogo kulinganisha na hifadhi zote nchini ikiwa na jumla ya kilomita za mraba 56.

Hifadhi imezungukwa na ukanda mwembamba wa misitu ya mlima unaokatizwa na miteremko mikali inayoingia katika mwambao wa ziwa Tanganyika ambapo hifadhi hii ipo umbali wa kilomita 16 kaskazini mwa mji wa Kigoma.

Hifadhi ya Taifa Gombe ni miongoni mwa makazi machache yaliyosalia ya sokwe mtu duniani,pia hifadhi hii ilipata umaarufu duniani hasa baada ya mtafiti wa tabia za sokwe mtu duniani Dk. Jane Goodall kufanya utafiti juu ya maisha na tabia za sokwe wa Gombe kwa muda wa miaka 40 na kuandika
vitabu kadhaa kuhusu wanyama hawa.

Kivutio kikubwa katika hifadhi ya Gombe ni sokwe mtu, kima wenye mikia myekundu, kima wa bluu, ziwa Tanganyika, msitu wa miombo pamoja na maporomoko ya maji ya kakombe. Wanyama jamii ya paka kama
chui na simba hawapo katika hifadhi hi na hivyo kuifanya kuwa salama kwa safari za miguu.

Likes:
0 0
Views:
446
Article Tags:
Article Categories:
TourismWildlife