Maajabu ya mti unaonyonga miti mingine

Waswahili wanasema tembea uone, na kuona ni kuamini, usemi huu unajidhihirisha Katika msitu wa Chome uliopo wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro ambapo Kuna mti ujulikanao kama Mvumo (Ficas) unaonyonga miti mingine mpaka kufa.

Watalii wengi wanaofika Katika msitu wa Chome huwa na shauku ya kujionea mti huo ambao kuota kwake kunategemea kujiviringisha katika miti mingine na kadri unavyoendelea kukua unaudhoofisha mti ambao umekuwa chanzo cha mti huo na hadi kuusababisha ukauke.

Amon Kihara ni muongoza watalii wa msitu wa Chome, uliopo Same, Kilimanjaro amesema kuwa kuna miti na mimea mingi katika msitu lakini mti wa Mvumo umekuwa ni kivutio sana kwa watalii wanaofika hapo kujionea uzuri wa msitu wa Chome wenye mimea mbalimbali na wanyama wanaopatikana hadi kwenye kilele cha mlima Shengena.

Kihara amesema kuna mti uitwao Igoma (Aningeria spp) ambao unatoa mlio ukipigwa kwa mujibu wa simulizi za zamani mti wa Igoma ulikuwa ukitumika kwa mawasiliano ya watu wa jamii ya Wapare kunapotokea dharura na wanataka kujulishana.

Msitu wa Chome una ukubwa wa kilomita za mraba zaidi ya (elfu sita) wenye mimea ya aina mbalimbali ambayo ni vivutio vikubwa katika Misitu huo pamoja na wanyama wakiwemo Mbega, Nguruwe pori na ndege wa aina mbalimbali.

Likes:
0 0
Views:
21
Article Tags:
Article Categories:
TourismWildlife