Mamba Katika hifadhi ya msitu Pindiro

Mamba ni moja kati ya vivutio vinavyopatikana katika Msitu wa Hifadhi wa Mazingira asilia Pindiro.

Mamba hao hujitokeza pembezeno mwa bwawa la viboko albino lililopo wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kila inapofika asubuhi na mchana ili kuota jua.

Mara nyingi wamekuwa wakikamata nyani kama chakula chao kwani hifadhi hii ya msitu Pindiro imetawaliwa na nyani wengi.

Mamba hawa wamekuwa ni kivutio cha pili katika bwawa la viboko albino kwa wageni, wanafunzi na watalii wanaotembelea hifadhi ya msitu Pindiro.

Likes:
0 0
Views:
593
Article Categories:
MuslimWildlife